Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

MAMBO USIYOYAJUA JUU YA VALENTINES DAY!

$
0
0
Leo ni tarehe 14 ya mwezi wa pili, ni tarehe maarufu ambayo watu wengi hasahasa vijana wanaitambua!!
NI SIKU YA WAPENDANAO…..
#Katika siku hii ya wapendanao kuna mengi sana ya kutambua yanashangaza lakini yatambue kwa sababu leo ndiyo siku yenyewe!!
#Zaidi ya kadi bilioni moja zinatumwa baina ya mtu na mwenzake ampendaye dunia nzima. Hii inasababisha siku hii kuwa siku ya pili ukiondoa sikukuu ya krismasi kuwa na ununuzi na utumwaji mkubwa wa kadi!!
#Huko nchini Finland ili kuweka usawa kwa wale wasiokuwa na wapenzi siku hii inaitwa SIKU YA MARAFIKI hasahasa wale marafiki waliotutangulia mbele za haki. Hivyo watu huitumia kiukweli kabisa kutoka moyoni kuwakumbuka wapendwa wao.
#Mnamo mwaka 1537 mfalme wa uingereza King Henry wa kumi na saba alitangaza rasmi kuwa Valentines day ni sikukuu rasmi nchini uingereza.
#Tumeona kuwa siku hii kadi nyingi sana hununuliwa na kutumwa zikiambatana na maua, kati ya asilimia 73 za wanunuzi wa hizo kadi ni wanaume wanawake asilimia 27 tu ndo hujihusisha katika kununua kadi. Wewe mwanamke unayenisikiliza umeshamnunulia umpendaye kadi? Au we unangoja kupendwa tu!!
#Huko nchini Marekani, wanawake zaidi ya asilimia 15 hukosa kabisa watu wa kuwatumia kadi hivyo hujinunulia kadi na kujiandikia majina yao kisha kujiwekea ndani. Na wewe ukikosa wa kukutumia jinunulie yako!!!

#Huko nchini Japani siku hii ilianza rasmi kutambulika mnamo mwaka 1936, lakini huko ipo kitofauti sana. Huko wanawake wananunua zawadi ya chocolate ambayo imeumbika mfano wa alama ya upendo kisha kumpelekea mwanaume,anaweza kuwa ni mpenzi wake ama si mpenzi wake. Kisha tarehe 14 mwezi wa tatu hiyo inakuwa siku ya malipo… wanaume kuwapa majibu wasichana!!!
#Siku ambazo maua yanatumika sana duniani ni siku ya akinamama na siku ya valentine!!!

#Katika nchi nyingine siku hii hutumika kutafutia wachumba, yaani msichana ukipewa zawadi mfano ya nguo ukiitunza basi unamaanisha umemkubalia aliyeituma kuwa katika mahusiano!! Na ukiitupa maana yake umemkataa…
Dah! Sasa upewe zawadi ya gari mwanadada kweli utaikataa???

Team papaso imechimba haya… lakini kwa ushauri jamani tusiitumie siku hii vibaya. Hasahasa kwetu Tanzania, vijana huigeuza kuwa siku ya kufanya ngono….. hiyo haikuwa maana halisi ya mtakatifu Valentine ambaye ndiye chanzo cha siku hii kusheherekewa duniani!!!
Unahitaji kumjua mtakatifu Valentine na chimbuko la Valentine… endelea kufuatilia chimbo la papaso na papaso kiujumla TBC fm J3 HADI iJumaa Ukiwa na Babamzazi Baba D'JARO ARUNG!!!

Share Kwa wengine Ukweli Huu!

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles