Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

KIZUNGUMKUTI!

$
0
0

Katika kijiji cha Matare wilaya ya Mugumu Serengeti, bwana Wambura alikamatwa kwa kesi ya kusingiziwa na kuhukumiwa kwenda jela miaka mitatu. Huku nyuma akiacha mke na
watoto wanne waliokuwa wanasoma. Hukumu hiyo ilimtesa sana kichwa chake, alitamani kila mtu anayemhisi kuwa ana makosa aingie katika moyo wake na kuupata ukweli. Alilia na umaskini wake, labda angepata wakili mzuri angeweza kumtetea, kumkosa wakili kukahalalisha kifungo hicho!!
Alikwenda gerezani huku akiumia sana rohoni.
Aliyaanza maisha mapya kwa shida sana, akawamnyonge kila mara na mwili ukapoteza afya kiujumla.
Huko gerezani alifanikiwa kupata rafiki aliyekuwa na cheo ama jukumu la uzikaji wa wafungwa hasahasa ambao hawakuwa na ndugu ama ambao ndugu zao huwa hawajitokezi pale gerezani. Mzikaji alijaribu sana kumtia moyo Wambura na kumwaminisha kuwa hiyo ilikuwa hatua tu ya maisha anapaswa kuizoea na siku moja ukweli utajulikana tu! Bwana Wambura maneno ya mzikaji hayakumuingia kabisa.. alizidi
kunyong’onyea.
“Siwezi kuvumilia kukaa gerezani miaka mitatu…..kama unajali kilio changu nisaidie nitoroke kwa namna yoyote ile ndugu yangu!!” Wambura alimsihi mzikaji.


SIKU MOJA mzikaji akamwambia Wambura kuwa msaada umepatikana. Lakini yataka moyo!!
“Nipo tayari kwa lolote ilimradi tu nitoke
humu!!” alijibu kwa msisitizo huku akimtegea sikio mzikaji.
“Msaada pekee wa kukutorosha humu ndani ni kwa njia ya jeneza… yaani mfungwa akifa mimi nakuunganisha naye kwenye jenerza…..” akashusha pumzi kisha akaendelea
“Wewe ukisikia kengele yamsiba, njoo mara moja kwenye chumba cha maiti, utakuta tayari sanduku liko katikati ya chumba linakuwa halijafungwa, funua mfuniko ingia ndani yake ulale pembeni ya maiti kwani
sanduku huwa kubwa la kutosha kila
aina ya maiti na hata miili miwili inaingia. Kisha nitakuja na kulipigilia misumari. Baada ya muda tutalipakia kwenye gari na kutoka kwenda nje ya gereza makaburini nikiongozana na baadhi ya wafungwa na maaskari magereza. Tutakuzika huko lakini baada ya
dakika 20 hadi 30 nitarudi kukufukua. Hautaweza kushindwa kupumua kwa dakika hizo, utatoka
ukiwa huru.”
JAPOKUWA wazo lilikuwa zuri lakini lilimtisha sana Wambura. Hata hivyo akaona afadhali afanye hivyo kuliko kukaa gerezani miaka mitatu bila kosa. Siku moja akasikia kengele ya msiba.
Akafanya kama alivyoelekezwa na mzikaji.
Akaenda na kuingia chumba cha
maiti. Kweli akalikuta sanduku, akiwa na hofu kuu akaingia na kulala pembeni ya maiti iliyokuwepo. Mara akasikia mtu ameingia na kulipigilia msumari sanduku. Muda mfupi
baadaye sanduku likainuliwa na kuwekwa kwenye gari. Gari likatoka nje ya gereza hadi makaburini. Sanduku likashushwa na kuwekwa kaburini na kuanza
kufukiwa. Wambura alijitahidi sana kuvumilia japo hofu ilizidi kutanda. Alimtegemea sana
mzikaji na alianza kumuona mkombozi wa maisha yake. Kama alivyoambiwa, akasubiri
dakika kumi, ishirini.. zikapita kimya!!
Dakika thelathini kimya. Joto nalo likazidi kuongezeka.
“Nitavumilia hadi afike…” alijisemea kisha akajiongezea kauli ya ujasiri.
“Kama nilitakiwa kuishi gerezani miaka mitatu kivipi dakika kadhaa za hapa kaburini
zinishinde” KWA kuwa alishakaa gerezani kwa muda kiasi akatamani kujua aliyekufa
ni nani… ni kweli aliogopa kuitazama maiti lakini aliona kama inatisha zaidi ikiwa imefunikwa vile kuliko ikiwa wazi. Akaifunua upande wa usoni… Kwa kuwa kulikuwa na giza nene alikodoa sana macho kuitazama.

LAHAULA!!! MACHO YAKAKUTANA
NA SURA YA MZIKAJI!!!
MZIKAJI ALIKUWA AMEKUFA NA
AMEZIKWA NA AHADI ZAKE ZA UKOMBOZI!!
________________

INGELIKUWA NI WEWE UNGEFANYA NINI...

KIZUNGUMKUTI....

Share Kama umeipenda Hii Story Ya Kweli.

Ila Pia Ukiwa na Story Kama Hizi Nitumie kwa email babamzazionline@gmail.com ili nitumie Kwenye Kipindi Cha PAPASO TBC fm Saa 1 jioni Hadi 4usiku J3 HADI Ijumaa.

Papaso ina segment Nyingi sana za Kuvutia sio la Kukosa Kusikiliza Ukiwa na DJARO ARUNGU.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles