Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Umewahi kukutana na usafirishaji wa magendo kwa njia hii?

$
0
0

Jamaa mmoja aliyekuwa akitokea China kwenda Hong Kong ametiwa nguvuni kwa kosa la kusafirisha simu kwa njia ya magendo, huenda kilichomponza ni namna alivyokuwa akitembea.



Watu walimshangaa kutokana alivyokuwa akitembea, wakawashtua maafisa wa Usalama, wakamfuatilia mtu huyo ili kujua sababu ya yeye kutembea hivyo.

Jamaa huyo alionekana akitembea kama amezidiwa na kitu kizito, alionekana akiwa amebeba mifuko miwili ya plastiki lakini isingemfanya aelemewe kiasi hicho, alipofika kwenye mashine zilizokuwa kwenye uwanja wa ndege kwa ajili ya ukaguzi zilipiga kelele na alipokaguliwa alikutwa na simu 94 za iPhone 5 na 6 alizokuwa amezifunga kwenye tumbo, mikono na miguu yake kwa gundi.



Simu hizo zilizuiwa huku Maofisa wa Usalama wakiendelea na upelelezi juu ya tukio hilo.







Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles