Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Pata Kujua Mengi Juu Ya Nyuki Wa Asali!

$
0
0
 
Huenda na wewe kuna kitu umewahi kukionja ukasema ni kitamu kama asali.
Kiukweli,asali ni tamu sana.


LAKINI asali hadi kukufikia wewe,tambua kuwa nyuki amefanya kazi ya ziada!!
Katika chimbo la Papaso leo tunamtazama nyuki wa asali na maisha yao kiujumla….
#NYUKI WA ASALI, hutembelea zaidi ya maua milioni mbili ili kuunda paundi moja ya asali.
#NYUKI WA ASALI huruka kimakadirio maili elfu hamsini na tano,ili kuleta nta ambazo hutumika kuunda hiyo paundi moja ya asali.
#Nyuki wa asali wamekuwa katika shughuli hiyo ya kuzalisha asali kwa zaidi ya miaka milioni kumi…
#Nyuki wa asali kwa wastani huunda nusu kijiko tu cha asali kwa maisha yake yote.
#Nyuki wa asali huchangia uchumi wa marekani kwa dola bilioni nane hadi kumi kwa mwaka!!
#Kuna wafugaji wa nyuki wasiopungua laki mbili nchini marekani.
#Nyuki wa asali ni wadudu pekee ambao wanaunda chakula kwa mwanadamu.
#Nyuki wa asali huruka kwa makadirio ya maili kumi na tano kwa saa.
#Hutanua na kushusha mbawa zake mara elfu kumi na mbili kwa dakika.
#Nyuki wa asali hutembelea maua zaidi 2000 kwa siku.
#Nyuki wa asali huwasiliana na wenzake kwa kutumia harufu na miondoko.
#Katika kipindi cha kiangazi,nyuki wa asali huishi kwa siku 28 hadi 35 tu kabla ya kufa.
#Kuna mizinga ipatayo milioni 3 na ushee nchini Marekani.
#Mzinga mmoja wa asali huwa na wastani wa nyuki 60,000.
#Malkia wa nyuki hutaga mayai 2000 kwa siku,ambayo ni wastani wa yai moja kila sekunde 45.Malkia hana kazi nyingine zaidi ya kutaga.
#Malkia wa nyuki mwenye afya njema hutaga kati ya mayai 175,000 hadi 200,000 kwa mwaka..
Leo Kwenye Chimbo La Papaso Nimekuletea Nyuki wa Asali.Naimani Umejifunza Kitu Msikilizaji Kwenye Papaso.







Chimbo la PAPASO inakuletea Vitu Adimu.

Sikiliza Kipindi Cha PAPASO Kila siku ya wiki j3-ijumaa Ili Uelemike na Kuburudika!


Kwenye PAPASO Unakutana Na Mtangazaji Mahiri D'JARO ARUNGU.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles