
Akibonga mawili matatu na paparazi wetu, Baby alisema suala hilo linahitaji umakini mkubwa katika uchaguzi na sifa anazozihitaji yeye ni upendo wa kweli na uhodari wa chumbani katika uwanja wa mahaba.
“Namsaka mwanaume mwenye sifa za kunizalisha, awe baba bora maana ishu ya kumpata mwanaume huyo si suala la mchezo lazima uwe makini ili mtoto wako ajivunie kwa mzazi aliyenaye, sichagui rangi ila awe mrefu na mwili uliojijenga, akiwa amenizidi umri au mdogo
freshi tu ilimradi aweze kazi,” alisema Baby.
Chanzo:gpl