
1. Maggie Vampire – Wanawake wa Dar – Wakazi
Â
Kwa miaka mingi wanawake wamekuwa wakitumika zaidi kupendezesha video za muziki duniani. Kazi hiyo imewawezesha baadhi ya video queens kuwa mastaa kwa kazi hiyo tu. Hii ni orodha yetu ya warembo 10 waliofanya vizuri zaidi kwenye video za wasanii wa Tanzania kwa mwaka 2014/2015.

Kwa wahudhuriaji wa fashion show, sura ya mrembo huyu sio ngeni kwakuwa amekuwa akionekana akipiga cat walks kwenye show kadhaa. Pia amekuwa akionekana kwenye matamasha makubwa mfano MTV Road 2 Mama 2014, Dar es Salaam kama usher. Amewahi pia kuigiza na AY kwenye tangazo la Samsung.
Â
2. Agnes Masogange – Msambinungwa – Tundaman f/ Alikiba

Umaarufu wa Masogange ulitokana na kushiriki kwenye video ya hit ya Belle 8, ‘Masogange’. Baada ya hapo alishiriki kwenye video za wasanii kadhaa na kufanikiwa kuwa miongoni wa ‘socialites’ wa Tanzania wanaondikwa zaidi kwenye magazeti ya udaku.

Mwanzoni mwa mwaka jana sakata la kudaiwa kupatikana na madawa ya kulevya kwenye uwanja wa ndege nchini Afrika Kusini lilimfanya awe kimya na kudai anaachana na kushiriki kwenye video. Hata hivyo mwaka jana alirejea tena kwenye video ya Tundaman.
3. Peninner Beda – Kolo Kolo – Mirror

Jina na sura ya Penniner bado lina ugeni kwa wengi lakini kwa wale waliiona video mpya ya Mirror, watakubali kuwa mrembo huyu atakuwa tishio kama atashiriki kwenye video zingine kali.

4.Zuhura Gora – The One – Hemedy & Jerry wa Rhymes

Zuhura aka Kamiligado alianza kufahamika kwenye video ya Professor Jay ‘Kamiligado’. Mwaka jana alitumiwa kuing’arisha video ya Hemedy na Jerry wa Rhymes.
5.Baby Nahiyyah – Togola – Dully Sykes, XO – Joh Makini / G-Nako, Umebadilika – Young Killer f/ Banana Zorro

Nahiyyah amefanya video nyingi zaidi katika kipindi cha hivi karibuni na ana nafasi ya kuonekana kwenye zingine nyingi.
6.Magdalena Olotu aka Maggie Minaj- Bishoo – Quick Rocka f/ Young Dee

Magdalena ni msichana aliyeenda hewani aliyetisha mno mno kwenye video ya Quick Rocka ‘Bishoo’. Pia anaonekana kwenye video ya Damian Soul ‘Ni Penzi’.

7.Sabrina – Bolingo – Bob Junior

Sabrina ni msichana aliyepewa jina la Rihanna wa Bongo na mwaka jana alitisha kwenye video ya Bob Junior.
8.Kaytesi – Jichunge – Baraka Da Prince, Adam Mchomvu – Au Sio

Kaytesi ni msichana mdogo na mrembo ambaye uwezo wake umeonekana kwenye ‘Jichunge’ ya Barakah Da Prince na zingine.

9. Sabrina (2) – Pesa – Mr Blue, Tummoghele – Izzo B

10.Carolyne Bernard – Ni Penzi – Damian Soul f/ Joh Makini

Carolyne ni Miss Universe Tanzania 2014 ambaye ajali ilimfanya ashindwa kuhudhuria mashindano ya Miss Universe na hivyo nafasi yake kuchukuliwa na mshindi wa pili. Kabla hajawa Miss Universe alikuwa ametumika kama model kwenye video ya Damian Soul.