
Mtu na mkewe walifika katika kituo cha Polisi kwa ajili ya kupeleka malalamiko ya mgogoro wa kifamilia waliokuwa nao, wakiwa wanatoa maeleo kila mmoja, mwanaume aliomba akachukue miwani yake ya kusomea katika gari, aliporudi alikuja akiwa na bastola, akampiga mke wake na kumuua, kisha akawanyooshea askari waliokuwa zamu, mwisho akajiua mwenyewe.
Watu hao walifikishwa katika kituo cha Polisi wakiwa katika magari tofauti, walikuwa na ugomvi katika nyumba yao Johannesburg ambapo Polisi walifika na kuamua kuwachukua kwenda nao kituoni hapo ili wakatafute suluhu ya ugomvi huo.
Credit:Millardayo.