MWANADADA mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, alionekana kivutio kikubwa kwa wapita njia baada ya kuonekana akiendesha pikipiki (Bodaboda) kwa kuimudu ipasavyo.
Mwanadada huyo ambaye alikuwa akifanya safari zake kati ya Mbezi na Kwembe jijini Dar,alionekana akiendesha kwa umakini wa hali ya juu huku akiwa na abiria.
(Habari/Picha: Gabriel Ng’osha/GPL)