Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

"NATAFUTA MIMBA KWA NJIA YOYOTE".....LINAH.

$
0
0

Estelina Sanga ‘Linah’.
STAA wa Bongo Fleva, Estelina Sanga ‘Linah’ juzikati ameweka wazi nia yake ya kusaka mtoto.


Akizungumza na  mwandishi wetu Desemba 9, mwaka huu jijini Dar, Linah alisema tangu alipoingia kwenye muziki hakuwahi kufikiria kushika ujauzito kwa kuwa alikuwa bado hajajiandaa kufanya hivyo.

Nyota huyo ambaye aliwahi kuzama  katika penzi zito la  staa mwenzake, Amin Mwinyimkuu alisema kuwa kwa sasa hali ni tofauti na anataka kuzaa iwapo atashika ujauzito.

“Nilipokuwa  katika uhusiano wangu wa kwanza hakuna hata siku moja niliyohisi kama nitakuja kutamani kupata mtoto maana mwenzangu aliponiambia tuzae nilimkatalia tofauti na leo hii natamani nishike mimba na ulimwengu wote ujue kwamba nina mimba,” alisema Linah.


Hata hivyo Linah alikwepa kuweka wazi uhusiano wake wa sasa na hakutaka kumwongelea Amin.


Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles