
Baada ya kuonekana kuwa mrembo wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu, amedanga kuhusu umri wake halali aliotakiwa kutaja ili Kamati ya
mashindano ya Miss Tanzania iweze kumruhusu kushiriki mashindano hayo au la, wadau wa tasnia ya urembo wanaomfahamu kwa karibu mrembo huyo wamekuwa wakizidi kutoa baadhi ya vidhibitisho vya mrembo huyo vinavyoonyesha umri halisi ambao ni miaka 25 badala ya ile 18 aliyoitaja.Aidha wadau hao wamezidi kwenda mbali zaidi kwa kuweka picha ya mrembo huyo inayoonyesha akiwa na mtoto wake jambo ambalo linazidi kuichanganya kamati ya mashindano hayo kwa kuona kuwa tayari huu ni mwaka wa tabu na kashfa kubwa kwao ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo.
Japo inawezekana ilishawahi kutokea kwa warembo kudanganya kuhusu umri na kuwa na watoto, lakini haikuweza kuwa na kishindo na kuvuta hisia za wengi kama ilivyo kwa mrembo huyu wa 2014.
Credit:Times fm