
Kupitia page zake za twitter na Instagram Brigitte pamoja na mengine ameandika >>> ‘Mazuri mengi yanawapita lakini inapotokea skendo mnajadili milele ndio maana hatuendelei, natamani tungeweka hizi nguvu za matusi kwenye vitu vya kujenga‘
Baada ya hiyo sentensi Brigitte alimuandikia Sitti kwa kusema >>> ‘Sitti usiwaruhusu watu wakuandame sana, ikizidi warudishie tu taji lao’
Kwenye tweets nyingine za wiki hii baada ya Sitti kutangazwa mshindi Brigitte aliandika ‘mngejua siasa za huko Miss World hata msinge jisumbua kumshambulia huyu msichana kiasi hicho, mtihani wa Miss Tanzania sio tu siku ya fainali ndio maana kunakua na camp ya siku 30′


Chanzo:Millardayo