
Alisema magonjwa hayo kwa sasa yameonekana kuchukua nafasi kubwa duniani na amewataka kuwa makini zaidi ili yasizidi kusambaa lakini pia kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya watu hasa wanaoishi maeneo yenye misitu kula nyama za nyani ambazo magonjwa hayo yanaaminika kuanzia huko, nao pia amewataka waache ili haya magonjwa ya ajabu yasije kwa binadamu.
Kitu kingine ambacho rais huyo alizungumza ni kitendo cha mabosi wa mahakama ya The Hague ya Uholanzi kumtaka rais mwenzake wa Kenya, Uhuru Kenyatta kuhudhuria kikao cha kujibu tuhuma dhidi yake kuhusiana na ghasia zilizotokea nchini kwake na kusema kililenga kudharau na kusitisha mkutano uliofanyika juzi nchini kwake.
Alisema pamoja na Serikali ya nchi hiyo kuomba rais Kenyatta kuhudhuria mkutano huo muhimu lakini mahakama hiyo ilionekana kukataa na kulazimisha ahudhurie katika kesi hiyo.
Hata hivyo Kenyatta alikanusha tuhuma za yeye kuhusika na ghasia zilizosababisha kupoteza maisha ya zaidi ya watu 1200 huku wengine zaidi ya laki sita wakikosa mahali pa kukaa mara baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu na jambo la mwisho alilozungumzia ni kuhusu timu ya Taifa ilo ambalo inakabiliwa na mchezo dhidi ya Togo ambapo aliwatakia kila la Kheri.