ASKARI watatu wa jeshi la Polisi wamelazwakatika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (Homso) iliyopo mjinisongea Mkoani humo wakiwa wanapatiwa matibabu ya majeraha ambayowaliyapata baada ya kushambuliwa kwa kitu kinachodhaniwa kuwa ni Bomu lakurushwa kwa mkono.
Tukio hilo limetokea September 16, 2014majira ya saa moja na nusu jioni katika kata ya Msufini karibu na daraja la Matarawe, wilayani Songea Mkoani Ruvuma ambapo watu watatu wasiofahamika walitupa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkonoambalo limetengenezwa kienyeji na kuwajeruhi askari hao watatuwaliokuwa doria.
Askari hao waliojeruhiwa ni WP. 10399 PCFelista aliyejeruhiwa mguu wa kulia kwenye unyayo na pajani ,G.7351 PC Ramadhani aliye jeruhiwa mguu wa kulia karibu na goti na tumboni upandewa kulia na G. 5515 pc John aliyepata majeraha katika mguu wa kuliachini ya goti na jeraha dogo tumboni.
Mganga mkuu wa Hospital ya Mkoa wa Ruvuma Dr. DanielMalekela ameeleza kutoa vipande vya bati na misumari katika majeraha ya askarihao na mpaka sasa wanaendelea na matibabu.
Alisema kufutia hali hiyo Jeshi la Polisi mkoaniRuvuma linaendelea na uchunguzi wa kina ili kuwakamata wahusika watukio hilo kwa hatua zaidi za kisheria.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Mhe. Saidi Mwambungu kasema amesikitishwa sana na kitendo hicho cha wahalifu kujeruhi askari tena kwa makusudi na amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha wanawasaka na kuwakamata.