Mashabiki wengine wa Brazil walionekana wakitoka kwenye uwanja wa Mineirao kabla ya muda kwa kudhihirisha uchungu uliowakabili kutokana na kutokuamini kilichokua kikitokea mbele ya macho yao, na wengine walidiriki kuondoka sehemu ambazo walikusanyika kwa moja kwa lengo la kuutazama mchezo huo kupitia runinga kubwa zilizofungwa kila kona nchini Brazil.
Lakini kituko cha kustaabisha kimeonekana katika mitaa ya Brazil, ambapo shabiki mmoja aliamua kuiadhibu runinga ya nyumbani kwake kwa madai ilimuonyesha namna timu yake ya taifa ilivyofungwa mabao saba kwa moja na Ujerumani.
Shabiki huyo ameonekana akiipiga runinga yake barabarani huku watu wake wa karibu wakisikika wakitoa sauti ya vilio ambavyo vilisababishwa na kadhia iliyowakumba.