
Millard Ayo (Mtangazaji machachari wa Clouds Fm) ameibuka kidedea kwa kunyakua tuzo mbili,
hivyo vikiwa ni vipengele vyote alivyoshindanishwa. Kilele cha Tuzo hizo kilikuwa ni Ijumaa hii
katika Serena Hotel, Dar es Salaam.
Kumbuka tu kwamba hivi majuzi nilikujuza kwamba Wema alikuwa mstari wa mbele kuwashawishi mashabiki kumpigia kura Millard Ayo, unaweza kujikumbusha hapa http://www.babamzazi.com/2014/06/millard-ayo-na-wema-sepetu-mhhh.html Je hatuwezi kusema Wema amechangia kwa kiasi kikubwa kushinda kwa Millard? Maana Wema ana fans wengi sana, na kama fans wake wote wamemuunga mkono kwa kutekeleza kile achowaomba nazani hilo halikuwa la kutowezekana. Picha kati ya waili hawa ikiendelea, basi ww.babamzazi.com itaendelea kuwajuza.
Tuzo alizonyakua Millard ni ya MTANGAZAJI WA REDIO
ANAYEPENDWA na KIPINDI CHA REDIO KINACHOPENDWA (Ambacho ni AMPLIFAYA)
Hongreara sana Millard Ayo kwa kunyakua Tuzo mbili
Washindi wengine katika vipengele mbalimbali ni kama ifuatavyo:
1 na 2 = MILLARD AYO
3.MTANGAZAJI WA RUNINGA ANAYEPENDWA = Salim Kikeke – BBC Swahili
4. KIPINDI CHA RUNINGA KINACHOPENDWA= Mkasi – EATV
5. MWANAMICHEZO ANAYEPENDWA=Juma Kaseja – Yanga
6. MUONGOZAJI WA VIDEO ZA MUZIKI ZINAZOPENDWA =Nisher
7. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIUME=My Number – Diamond
8. VIDEO YA MUZIKI INAYOPENDWA YA MWANAMUZIKI WA KIKE= Yahaya – Lady Jaydee
09. MUIGIZAJI WA KIUME KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA= King Majuto
10. MUIGIZAJI WA KIKE KWENYE FILAMU ANAYEPENDWA =Elizabeth ‘Lulu’ Michael
11. FILAMU INAYOPENDWA =Ndoa Yangu