Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Sare ya Japan na Ugiriki yaifungulia mlango Ivory Coast kuelekea 16 bora.

$
0
0
Baada ya mashabiki wa soka barani Afrika kuumizwa na hatua ya kufungwa kwa Ivory Coast katika mchezo wajana dhidi ya timu ya taifa ya Colombia, timu za Japan pamoja na Ugiriki zimeshindwa kutambiana katika mpambano uliochezwa usiku wa manane huko Arena das Dunas, mjini Natal.

Mchezo huo wa kundi la tatu ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bila kufungana, hali ambayo inaendelea kulifanya kundi hilo kuwa gumu baada ya timu ya taifa ya Colombia kufaulu kucheza hatua ya 16 kufuatia ushindi wa mabao mawili kwa moja waliouchuma kutoka kwa Ivory Coast hapoa jana jioni.
Kundi hilo bado linatoa nafasi kwa Japana, Ugiriki pamoja na wawakilishi wa bara la Afrika Ivory Coast ambapo timu moja ambayo itaungana na wakulima wa kawaha timu ya taifa ya Colombia itafahamika mara baada ya michezo ya mzunguuko wa tatu itakayochezwa juma lijalo.
Michezo hiyo itashudia timu ya taifa ya Ivory Coast ikipambana na Ugiriki na timu ya taifa ya Japan itachakachuana na Colombia mnamo June 24.
Hii leo mshike mshike wa fainali za kombe la dunia unaendelea tena kwa michezo mitatu ambapo mchezo utakaochezwa mishale ya saa moja jioni kwa hapa nyumbani utakuwa ni ule wa kundi la nne kati ya mabingwa wa dunia wa mwaka 2006 timu ya taifa ya Italia dhidi ya Costa Rica.
Mchezo utakaofuata mishale ya saa nne usiku utakuwa ni wa kundi la tano ambapo mabingwa wa soka duniani wa mwaka 1998 timu ya taifa ya Ufaransa watawakabili Uswiz.
Na kisha mchezo mwingine wa kundi hilo utafuatia mishale ya saa saba usiku kati ya Ecuador dhidi ya Honduras.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles