Mbasha (Mume wa Flora) akiingizwa Maabusu |
misingi husika ya imani hiyo. Flora Mbasha ni mwimbaji wa injili na kwa mujibu wa imani yake, tunajua "AMEOKOKA"
Labda turudi katika misingi ya ukristo hususani kwa watu WALIOOKOKA, je ni mambo gani ambayo tunategemea kutoka kwa watu hao wenye imani ya juu ya dini yao. Tukumbuke tu kwamba WALIOOKOKA ndio wanasadikika kuwazidi kiimani wakristu wengine (ambao hawajaokoka)
Mimi sio gwiji wa imani ya Kikristo ila naamini kauli hizi ni mbili zinahusika sana na inatakiwa zifuatwe na wakritu wote (tena inatakiwa zisimamiwe vilivyo hasa na WALOKOLE, akiwemo Flora Mbasha). Kauli hizo ni hizi hapa;
1. MSAMEHE MWENZAKO (ALIYEKUKOSEA) SABA MARA SABINI
2. MPENDE JIRANI YAKO (MWENZAKO) KAMA UNAVYOIPENDA NAFSI YAKO
Maswali yangu kwa Flora Mbasha ni haya;
1. Je umewahi kumsamehe mumeo mara ngapi?
2. Ulokole/ukristu gani ambao wewe unautangaza kupitia nyimbo zako wakati unashindwa kumsamehe mumeo?
3. Wakristu wanaamini pia kauli hii "USIMHUKUMU MWENZAKO", je wewe umekuwa nani hadi leo unamhukumu mumeo? Je wewe umechukua nafasi ya Mungu?
FLORA MBASHA, TAFAKARI UJUMBE HUU MARA NYINGI AKILI MWAKO NA UFANYE MAAMUZI SAHIHI JUU YA MUMEO.
Mchambuzi Mahiri wa Mambo