Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Wamuua mdogo wao wa kike mbele ya wazazi wao na kuchoma mwili kisa mapenzi.

$
0
0
Matukio ya ajabu yanaendelea kuripotiwa duniani huku mengine yakitokana na uamuzi wa ajabu unaoendeshwa na hasira za kijinga .
Msichana mmoja wa kijiji cha Sabhapur, Aligarh, India  aliyetajwa kwa jina la Devendri ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa na kaka zake watatu mbele ya wazazi wao baada ya kurudi nyumbani na kugundulika kuwa alikuwa ametoka kwa mvulana wa kijijini kwao na alikaa nae kwa muda wa siku mbili.
Kwa mujibu wa Hindustantimes, msichana huyo aliondoka nyumbani kwao June 14 na kurudi June 16 ambapo aliwakuta kaka zake wakiwa na hasira na baadae kumpiga risasi.
Baada ya tukio hilo waliamua kumchoma moto ili kupoteza ushahidi lakini kabla hawajafikia mbali ndipo polisi walipopata taarifa na kufika katika eneo la tukio hawakuwakuta watuhumiwa hao.
Polisi wameiambia HT kuwa wanawasaka watuhumiwa hao ambao ni kaka zake Dharmendra, Bhoora na Bhola.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles