
wanategemea sana kuutumia na kuacha magari yao nyumbani na kujikuta wamewahi town na kumaliza shughuli zao manake hamna foleni.
Dar es salaam likiwa jiji la tisa kwa ukuaji duniani huku kwa Afrika likishika nafasi ya tatu, limekua na foleni kubwa ambazo mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) inasema huwa kila siku inapatikana hasara ya shilingi BILIONI TATU kutokana na foleni Dar es salaam.

Elisha Elia alimuuliza Mwakyembe… Je umeme wa bongo tunavyoufahamu na historia yake utafaa kuuwezesha usafiri huo wa Treni kufanya kazi yake? manake treni hizi za kasi zinatumia umeme.
Akajibiwa ‘hawatotumia umeme wa TANESCO, watatumia umeme wa solar na vyanzo vingine vya umeme ili isitokee treni ikasimama katikati manake umeme ni lazima uwepo kwa saa 24′
