
Kadi ya njano aliyoonyeshwa kiungo huyo wa kutoka nchini Hispania ilikuwa ya tatu mfululizo na hivyo ataukosa mchezo wa fainali ya michuano hiyo dhidi ya klabu ya Atletico Madrid uliopangwa kuchezwa May 24 mjini Lisbon nchini Ureno.
Bodi ya nidhamu ya shirikisho la soka barani Ulaya UEFA, limeiweka kapuni rufaa hiyo baada ya kutorishishwa na sababu zilizoainishwa na klabu ya Real Madrid ya kutaka Xavi Alonzo aruhusiwe kucheza mchezo huo ambao utakua muhimu kwa klau zote mbilia mbazo zinatoka mjini Madrid nchini Hispania.
Kufuatia UEFA kuendelea na msimamo wa kuiacha adhabu kwa Xavi Alonso, kuendelea, meneja wa klabu ya Real Madrid Carlo Ancelotti, huenda akafanya maamuzi ya kumtumia kiungo kutoka nchini Ujerumani Sami Khedira, ambaye alikuwa majeruhi ama Asier Illarramendi Andonegi.
Wakati huo huo klabu ya Real Madrid imeendelea kujipunguzia matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi ya nchini Hispania nchini huu, baada ya kushindwa kuibuka na ushindi katika mchezo wa ligi hiyo uliochezwa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Real Valladolid.
Mchezo huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao moja kwa moja na hivyo yameifanya Real Madrid kuendelea kubaki katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya La Liga kwa kufikisha point 84 tofauti ya nne dhidi ya vinara wa ligi hiyo Atletico Madrid.
Endapo Real Madrid watahitaji kutimiza malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu huko nchini Hispania, itawalazimu kusaka ushindi katika michezo yao miwili iliyosalia kwa msimu huu dhidi ya Celta de Vigo na Espanyol huku wakiiombea Atlertico Madrid ifungwe na FC Barcelona.