
Kwenye dakika 14 za interview ya ABC amesema Donald ambae kwa sasa anajisikia mpweke, anatakiwa kuomba msamaha japo haijulikani ni lini ila Mungu pekee ndio anajua.
Anasema uhusiano wa kimapenzi ulianza wakati akifanya kazi chini ya bilionea huyu na ni mapenzi ambayo ilifikia kipindi watu walikua wanamshangaa au wanashindwa kuelewa uhusiano wao.
V Stiviano amesema bado anampenda Sterling ila hayuko nae inlove, anampenda kama baba…. Sterling kiumri ana miaka 80 na yeye ana umri wa miaka 31.
V anasema amekua msaidizi wa Donald na kwamba chanzo cha yeye kutembea akiwa amejiziba uso toka hii ishu itokee ni ili asiongee na Waandishi ambao wamekua wakimuandama wasimpate, hakutaka kuongea chochote sababu alikua na machungu na kwamba ni ngumu kuona mtu unaemjali akiwa kwenye maumivu.
Anasema Waandishi wa habari wamekua wakikosea na kuuliza watu kuhusu yeye lakini kosa kubwa wanalolifanya ni kwamba wanauliza watu ambao sio sahihi kuulizwa kuhusu yeye. (wrong people)
Pamoja na yote yaliyotokea V ameushangaza ulimwengu kwa kumtetea Sterling kwamba sio mbaguzi na kama angekua mbaguzi basi asingetoa msaada ambao ameutoa mpaka sasa kwa watu mbalimbali… ‘kupitia matendo yake ameonyesha kwamba sio mbaguzi na ni mtu mkarimu’

Kwenye sentensi nyingine V anasema sehemu ya sauti iliyosikika Donald akitoa
maneno ya kibaguzi kuhusu watu weusi ni dakika 15 tu kati ya saa kadhaa za
maongezi ambayo dunia haijazisikia.