Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

TABIA NZURI ZA WANAWAKE ZIMEHARIBIWA NA MAVAZI YA UCHI WANAYOVAA.

$
0
0
Kwanza ningependa tufahamu tabia nzuri,maadili mema,usikivu na Uelewa vinajengwa na malezi bora kutoka kwa wazazi na wapili walimu wetu mashuleni na tatu jamii inayotuzunguka wakiwamo marafiki na wengineo wanaokuzunguka...
Napenda kurudi kwenye pointi ya msingi.Tabia nzuri za wanawake zimehalibiwa na mavazi ya uchi wanayovaa..Hii ni kweli kabisa kwenye dunia ya leo iliyojaa utandawazi uliopelekea leo wanawake wakitanzania kuiga ata yale yasiyoendana na mila zetu wala taifa letu
Uvaaji mbovu wa dadazetu umesababisha kupunguza heshima zao na kuonekana kituko mbele ya jamii.kuna mambo mengi sana ya msingi ya kuiga kwenye dunia ya leo kama tutajiheshimu na kufata yale yaliyo na msingi.Kuepuka makundi yasiyokuwa na manufaa kwetu asa vijana.

DINI..Hiki ni kitu cha msingi sana tukizifata dini zetu na kuziheshimu.Ndio msingi bora na wapekee utaotutoa kwenye shimo ili lililokosa maadili na tabia chafu zinazoendelea kujengwa na shetani.mambo yanazidi kuwa machafu ndani ya jamii baada ya kuzisahau dini zetu na mafundisho bora kutoka kwa wazazi wetu
 KWENDA NA WAKATI.. Hapa sasa ndio vijana wengi tunashindwa kuelewa huu msemo.ni kweli kabisa vijana tunahitaji kwenda na wakati ila sio kuiga yanayohalibu wakati.nafikili hapo tumeelewana..NI VIZURI KWENDA NA WAKATI ILA SIO KUIGA YANAYOHARIBU WAKATI.. kuna mambo mengi ya kuiga.hapa sasa unahitajika uelewa.vitu kama Laptop.Tv na vinginevyo vinavyochangia kuhalibu maadili ni vizuri sana na muhimu sana kama vitatumiwa kwa kazi muafaka.Ila leo kumeibuka kundi kubwa la dadazetu kutumia vibaya izi laptop kuiga maadili mabaya kutoka ngambo kama uvaaji wa uchi kabisa na kuzitumia vibaya kuweka picha zao za uchi kwenye mitandao ya jamii ni aibu sana
DADA ZETU WAKITANZANIA.. Ni vizuri dadazetu kujifunza na kukubali kubadilika na kujiheshimu..mimi naamini sana wote tumetoka kwenye maadili mazuri sana sisi kama vijana wakitanzania..mambo ya digital mjalibu kwenda nayo na kujitahidi kujifunza yale yaliyo mema.Tabia chafu za kuiga sisi kama.Watanzania hatujazaliwa nazo ila tumezikuta na mwisho wake zimetuingia na kusababisha kuhalibu sifa nzuri ya mwanamke.Huu uvaaji wa uchi umesababisha leo dadazetu kukosa sifa nzuri za mwanamke na kuonekana na mwenye tabia mbaya kwenye jamii
USHAURU.. Dadazetu mjalibu kumludia Mungu na kuheshimu wazazi wetu na jamii yote inayotuzunguka.Wazazi mjalibu kukemea tabia mbaya na uvaaji mbovu kwa hawa dadazetun na jamii yote iliyokuwa na msimamo ndio inayojenga taifa bora.Watanzania ili kujenga viongozi bora tukemee hayo yanayoendelea sasa na ili kupata Wanawake bora wenye kujiheshimu tukataze uchafuuu.....
WEWE KAMA MTANZANIA AMUA SASA PIGA TABIA CHAFU ZA DADA ZETU ZIMESABABISHA KUCHAFUA SIFA NZURI WALIZOPEWA NA MWENYEMUNGU

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles