
Abiria hao wamesimulia katika nyakati tofauti lakini kwa mujibu wa BBC maelezo yao yamekuwa yakifanana.
“Kwa kweli kulikuwa na sauti kubwa na meli ghafla ikaanza kuegemea uapande mmoja. Watu walikuwa wakihangaika kukimbilia maeneo ya juu ya meli, lakini ilikuwa vigumu kufanya hivyo kutokana na meli kupinduka.” Amesema Kim Song-Muk.
Kikosi cha walinzi cha Pwani ya Korea kusini kimesema abiria watatao mia tatu hawajulikani walipo. Imeripotiwa kuwa watu wawili wamepoteza maisha na watu 164 wameokolewa.
Bado haijafahamika chanzo kilichosababisha kuzama kwa meli hiyo ambayo ilikuwa na jumla ya watu 460 na wengi wao wakiwa wanafunzi wa sekondari waliokuwa wakielekea katika kisiwa cha Jeju, nchini Korea Kusini.