Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Q Chilla aelezea ujio wake mpya na collabo za kimataifa alizofanya, anafanya kazi na producer mpya kutoka Lebanon.

$
0
0
Q Chilla ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa amejipanga kurudi katika game kwa nguvu hivi karibuni na kwamba amemaliza hatua ya awali ya kuwaomba radhi wadau wa muziki ambao aliwakosea alipokuwa katika hali ya matumizi ya madawa ya kulevya.
“Mtu yeyote akiwa katika hali mbaya ya fikra potovu, kwenye madawa kwenye msongo wa mawazo anakuwa hayuko normal psychologically kwa hiyo vitu vingi vinaweza kutokea ukamuona ni mtu sio ambaye anafanana na wenzake. Kwa hiyo niliamia kwenye amani kuset mambo vizuri.” Amesema Q Chilla.
“Kwa hiyo nilikutana na wadau mbalimbali wa muziki kuzungumza. Jamani mimi ni ndugu yenu, naweza kuwa nimekosea hapa na pale lakini pia nahisi nina nafasi kubwa katika jamii na tasnia hii ya muziki. Na nina malengo na familia na watoto wananitazama.”
Ameeleza kuwa hata wale ambao hakuwafikia anaamini wamemsamehe pia na kwamba baada ya hapo alijisikia yuko huru na kuanza kuangalia project zake.
Mwimbaji huyo amesema ameshiriki katika kazi mbalimbali za kimataifa ikiwa ni pamoja na video aliyofanya na msanii mkubwa kutoka Ufaransa na amefanya production Ufaransa na kumalizia Zanzibar na kwamba iko katika hatua za mwisho.
“Halafu nikafanya video nyingine tena na msanii wa kimataifa toka Ethiopia Addis Ababa chini ya director mkubwa sana Afrika ambaye alinipa connection hii na akanishuti kwa gharama zake tukaenda Ethiopia lakini tunabidi tumalizie hapa shots za mwisho.” Ameeleza.
Hivi sasa mwimbaji huyo amepanga kutanguliza audio kati ya nyimbo mbili alizozitaja kuwa ni Red Carpet au Power of Love aliyofanya na producer mpya kwa Tanzania, mtanzania aliyekuwa akiishi Uingereza na Lebanon.
“Kuna producer mpya kutoka Lebanon amekuja hapa…amesoma Uingereza na Lebano lakini ni mtanzania ambaye anaishi Arusha, amekuja hapa amependa kazi zangu akasema ‘Q Chief naona unapenda sana kwenda International, naona una dream za kufika mbali. Nimekuwa nikifuatilia story ya maisha yako, ups zako and downs nahisi kwamba mzigo huu unaweza kukufikisha sehemu fulani. Kwa hiyo kuna mzigo unaitwa Power of Love unakuja.”

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles