
Mapema wiki iliyopita iliripotiwa kwamba Diarra, 29, alijiunga na katika vita inayoendelea Syria baada ya kutolewa kwa video inayomuonyesha mtu akiwa kavaa mask — ambaye alijitambulisha kwamba ni Lassana Diarra.
Hata hivyo, kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa, ambaye aliwahi pia kuitumikia Portsmouth na Chelsea, ametoa taarifa rasmi kupitia wakili wake na kusema kwamba hahusiki kabisa kabisa na video hiyo.
“Lassana anakana rasmi kuhusika na video hiyo. Hajawahi kukanyaga nchini Syria. Ni ujinga na yeye sio mfuasi wa jihad, ni mwanasoka anayeichezea Lokomotiv Moscow,” alisema mwanasheria wa mchezaji huyo.