
Akiongea na kituo kimoja cha radio jana, Belle amesema ndio maana mara nyingi huwa yupo Morogoro na familia yake ambapo pia wana mtoto mmoja.
“Ni mchumba lakini kwa safari ambayo tumetoka tayari ni mke wangu,” alisema Belle.
Aliongeza kuwa hivi karibuni atafunga ndoa na mchumba wake huyo aitwaye Nia.
Kwa sasa Belle 9 ameachia single mpya iitwayo Wanitamani/Wanitaka.