Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all 2632 articles
Browse latest View live

HUYU MSANII WA FILAMU ZA BONGO AMESEMA AACHWE AVAE ATAKAVYO.

$
0
0

“Waniache bwana, sijakataa kama mimi ni mke wa mtu lakini pia nipewe uhuru kwani najitambua,” alisema.



Mkali wa sinema za Kibongo, Aunt Ezekiel pichani.
Akifafanua kauli yake mbele ya kinasa sauti chetu, Aunt alisema watu wengi wamekuwa wakimtaka avae kistaarabu kwa kuwa ni mke wa mtu.
CREDIT:GPL

KABURI LA SHEIKH YAHYA HUSSEIN LAFUKULIWA.

$
0
0

Makaburi mawili ya Sheikh Yahya Hussein na Sheikh Kaseem Bin Jumaa yamevunjwa na mgambo wa jiji saa nane usiku eneo la Tambaza, makaburi ambayo yana muda mrefu katika eno hilo.

Hata hivyo haijajulikana chanzo cha kuvunjwa kwa makaburi hayo.
Wakiongea na waandishi wa habari baadhi ya wafanyabiashara wa maduka ya vyakula eneo hilo wamedai kuwa, walifika asubuhi na kukuta hali hiyo ya kuvunjwa kwa vibaraza vya maduka yao pamoja na kuvunjwa kwa makaburi hayo mawili ya watu masheikh mashuhuri hapa nchini.

JOHARI AFUNGUKA "OSTAZ HANA PESA WA HADHI YA KUNIOA MIE"

$
0
0
Staa mkubwa wa sinema za Bongo, Blandina Chagula ‘Johari’ ameingia kwenye vita ya maneno na bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma ikiwa ni siku chache tangu jamaa huyo alipotangaza kumuoa mwanadada huyo.


Wakizungumza na Risasi Jumamosi kwa nyakati tofauti, kila mmoja alitoa la moyoni huku Johari akionekana kukasirishwa mno na ishu hiyo.
KILICHOMPONZA JOHARI
Ilidaiwa kuwa baada ya Ostaz kutangaza kwamba atafunga ndoa na Johari, vyombo mbalimbali vya habari na mitandao ya kijamii vililichukulia jambo hilo kwa ukubwa wake kwani mwanadada huyo hakufunguka sawasawa.
WENGINE WADAI KULIPA KISASI
Habari zinasema baada ya ishu hiyo kugeuka habari ya mjini ilidaiwa kwamba labda Johari aliamua kufanya hivyo kwa kuwa mkurugenzi mwenzake wa RJ Film Production ‘RJ’, Vincent Kigosi ‘Ray The Greatest’ naye alidaiwa ‘kuchepuka’ na Chuchu Hans.

Kuenea kwa habari za Johari kuolewa na Ostaz kulimsababishia usumbufu mkubwa mwanadada huyo kutoka kwa ndugu, jamaa na marafiki wakihoji ukweli wa ishu hiyo ili kujiandaa na cherekochereko.
MADAI YA AWALI YA OSTAZ
Katika maelezo yake ambayo yapo kwenye rekodi zetu, Ostaz alidai kuwa Johari anajua kila kitu kwani walifahamiana kitambo hata kabla ya mrembo huyo kujuana na Ray.
Hakuishia hapo, Ostaz alidai kuwa tayari amemfungulia Johari kampuni ya kutengeneza sinema pamoja na vifaa vyote hivyo yupo kwenye mishemishe za kumuoa.
JOHARI SASA
Ili kuondoa utata huo, gazeti hili lilimtafuta Johari kwa udi na uvumba na kutaka kujua undani wa ishu hiyo ambayo imezua maswali mengi hasa kwa mashabiki wake.Johari: Sijawahi, sina na wala siwezi kuwa na uhusiano na mtu mpuuzi kama yule (Ostaz Juma). Mwanzoni nilidhani utani, nashangaa imekuwa ishu kubwa.

Risasi Jumamosi: Kwani hufahamiani na Ostaz? Mbona anasema anakujua tangu unaishi Mburahati, Dar na enzi ukiwa Kaole?
Johari: Ni kweli Ostaz alikuwaga anakuja pale Kaole tulipokuwa tunafanya mazoezi lakini si yeye waliokuwa wanakuja ni wengi.
Risasi Jumamosi: Je, hajawahi kuleta maombi ya kukuoa?
Johari: Hakuwahi kunitongoza ila kila nilipokutana naye nilikuwa najua kwa kumwangalia tu machoni. Alikuwa anaonesha kabisa ananitaka lakini hakuwahi kunitamkia.
“Hajawahi kuniambia anataka kunioa. Kwanza mimi ni Mkristo. Sina ndoa mbili. Siwezi kuolewa mke wa pili na mpuuzi kama yeye.
Risasi Jumamosi: Je, zile picha zilizosambaa ukiwa umepozi kimahaba na Ostaz zilitoka wapi?
Risasi Jumamosi: Ilikuwa nje ya RJ, nilipiga picha na watu wengi kama Dogo Janja akiwemo na huyo Ostaz. Nilipigwa na butwaa nilipoziona mitandaoni eti nina uhusiano na Ostaz huku naye akiulizwa na kudai ni kweli.
“Kwani kupiga picha na mtu ndiyo tayari mmekuwa wapenzi au wachumba? Labda yeye anachukulia hivyo kwamba ukishapiga picha na mwanamke tayari anakuwa mpenzi wako.”
Risasi Jumamosi: Kuhusu dini, Ostaz alisema atakubali uwe Mwislamu na jina lako litakuwa Rahma. Je, alishakuambia juu ya hilo?

Johari: Hajaniambia, hata  hivyo, sina mpango wa kubadili dini ili niolewe na yeye.
Risasi Jumamosi: Vipi kuhusu Ostaz kukufungulia kampuni na vifaa vya kutengenezea sinema?
Johari: Mh! Achana na kampuni au vifaa, hata simu tu hajawahi kuninunulia, kwanza hana fedha. Halafu ajue kabisa kwamba mimi ni tofauti na hao wasanii wengine wanaoishi kwa kutegemea kuhongwa. Mimi ni super woman, siku hizi huwa fedha kwangu ni makaratasi. Huyo Ostaz ana fedha gani?
“Haniwezi, mimi siyo kama hao watoto anaowadhalilisha kwa kuwapigisha magoti na akome kabisa kutumia jina langu kama daraja. Hakuna kitu ninachochukia kama mtu kutaka kutumia jina langu kujitafutia umaarufu, ana hadhi gani ya kuwa na mimi, akome kabisa, mimi nimesota, ninyi Global mnajua.”
Risasi Jumamosi: Umekana kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Ostaz, je, una mchumba au mpenzi?
Johari: Mimi ni mwanamke niliyekamilika. Nina mchumba na ‘soon’ nitamtambulisha kwa mashabiki wangu. Lakini ijulikane kuwa siyo Ostaz kwani hawezi kuwa mchumba wangu.
Risasi Jumamosi: Au unataka kurudi kwa Ray?
Johari: (mshtuko) hivi ni nani aliwahi kutamka kwamba mimi na Ray ni wapenzi. Hapana, siyo Ray.
Risasi Jumamosi: Kwani Ray ni nani kwako?
Johari: Ray ni mkurugenzi mwenzangu wa RJ. Nje ya kazi tuna maisha yetu mengine.
Risasi Jumamosi: Je, ni mtu maarufu?
Johari: Nimeshasema nitawatambulisha subirini. Unajua mimi siyo mtu wa matangazo. 
Baada ya kumsikia Johari, gazeti hili lilimgeukia Ostaz ambaye hakupatikana, lakini rafiki yake wa karibu alidai kuwa Johari amechanganyikiwa kwani Ostaz alikuwa amuoe kweli lakini hamuelewi mwenendo wake wa sasa.
“Johari amechanganyikiwa,” alisema rafiki huyo.

Credit:GPL


KAZI KWELI KWELI KATIKA BUNGE LETU!

$
0
0
Ni kama anasema "Mzee embu weka pozi moja kali hapo nikufotoe picha kali ya kuweka Facebook , Hapo hapo Kaka...."

ETI HUYU DADA NDIO KIBOKO WA AGNES MASOGANGE.

$
0
0
MODO anayesifika kwa kujaliwa makalio, Agnes Jerald ‘Masogange’ amepata mpinzani lakini akachomoa kuhusu suala la kufunikwa.


Masogange alizungumza hayo juzikati baada ya kukutana na mrembo aliyejulikana kwa jina la Samia pande za Sauz.

Walipopiga picha ya pamoja, Masogange alipinga baada ya paparazi wetu kumhoji.
“Hawezi kunizidi mimi, hatari wewe,” alijisifu Masogange kwa paparazi wetu.
JE wewe unasema nani zaidi hapo kwa pic?

Gari Na Shetta Baada Ya Ajali Iliyosababisha Gari Kupinduka Mara 3.

$
0
0

Msanii Shetta jana mida ya saa kumi na mbili jioni amepata ajali mbaya ya gari eneo la
Minjingu/Monduli akiwa anaendeshwa kwenye gari aina ya Noah. Imegundulika na MrInfo kuwa ajali hii imemsababishia Shetta majeraha machache kwenye mikoni,miguu na moja kichwani.
Shetta anasema ni bahati sana kutoka hai kwani gari ilipindika mara tatu.
IMG-20140412-WA0000 IMG-20140412-WA0001
CREDIT:Sammisago.com

Makundi Ya Nusu Fainali Ligi Ya Mabingwa Ulaya Ndio Haya.

$
0
0

Makundi Ya Nusu Fainali Uefa yamepangwa na game zitaanza April 22, Bayern Munich itacheza na Real Madrid,

 Chelsea inakutana na Atletico Madrid katika game za nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, fahamu hii itakuwa na game nane sababu mtoano unahitaji game mbili, home and away.
Endelea kufuatilia habari za michezo na burudani kupitia twitter na instagram @sammisago, Asante
game 2game 3game 5

Download Na Sikiliza Wimbo Mpya Wa Wagosi Wa Kaya – Bao.

$
0
0

Wagosi Wa Kaya wamevunja ukimya baada ya miaka 8 bila kuwa na wimbo wao pamoja,

Wagosi kwenye interview na MrInfo, wamesema hawajarudi kwenye game sababu ya kampeni za uchaguzi iliwapate show ila ndio wakati wa kuendeleza walipoachia miaka 8 nyuma.
Kuhusu tofauti kati yao Mkoloni anasema Wagosi Wakaya ni familia na hawawezi kuwa na tofauti za kudumu, wameyamaliza.


Watu 56 wanusurika ajali ya ndege Dar.

$
0
0
Watu 56 wamenusurika baada ya ndege ya Shirika la Ndege la Kenya(Kenya Airways) waliyokuwa wakisafiria kupata ajali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Dar es Salaam(JNIA) jana ilipokuwa ikitua.
Kamanda wa Polisi Viwanja vya Ndege, Kamiishna Khamis Selemani alithibitisha kutokea kwa ajali akieleza kuwa ilisababishwa na rubani kupoteza mwelekeo na kushindwa kuona njia sahihi kutokana na mvua kubwa iliyokuwa ikinyesha uwanjani hapo.
Ndege hiyo yenye namba 5Y-FFT aina ya Embrarer 190 yenye uwezo wa kubeba abiria 90 ilipata ajali hiyo mchana ikiwa na abiria 49 na wafanyakazi saba.
“Tulipata taarifa za kuanguka kwa ndege hiyo majira ya saa 8:26 mchana. Ndege hiyo imepata hitilafu katika injini yake ya upande wa kulia ambayo imebonyea pamoja na kupasuka ubavuni,” alisema Selemani.
Kamanda huyo aliongeza kuwa pia tairi la mbele la ndege hiyo limepasuka baada ya kujigonga, lakini hakuna kifo kilichotokea wala majeruhi waliohitaji matibabu.
“Haitoweza kuruka kabla ya marekebisho kwani hewa itaingia ndani jambo ambalo haliruhusiwi kwa usafiri wa angani katika viwango vya kimataifa,” aliongeza Seleman.
Katika hatua nyingine, ndege ya Shirika la Ndege la Emirates, ilishindwa kutua kwenye uwanja huo jana kutokana na mvua hizo, hivyo kulazimika kwenda kutua Uwanja wa Ndege wa Mombasa nchini Kenya.

MWISHO MWAMPAMBA NA UJUMBE MZITO FACEBOOK.

$
0
0
Huenda mwakilishi wa mara mbili wa Tanzania kwenye shindano la Big Brother Africa, Mwisho Mwapamba anaufurahia zaidi wimbo wa Pharrell Williams, ‘Happy’ kuliko mtu mwingine yeyote.


“Nashukuru sanaa mungu kwa kunipatia kazi mpya kitu kipya cha kujifunza! pia biashara zaenda sawa ! new house ni mzuka sanaa uhuru wa kutosha japo umeme bado ila ndio mambo yangu hayo. pia family ipo njema kiafya so im very happy! just miss my kids na wife kuspend muda pamoja but its all good sikuzinaenda kwa kasi na when u fight the good fighty, u fight good,” kupitia Facebook, ameandika Mwampamba ambaye kwa sasa anaishi nchini Namibia na mke wake Meryl Vuyeya Mwampamba (japo kwa sasa yupo nchini).

JUMA NATURE ALIA NA JOKATE MWEGELO.

$
0
0
Chelewa chelewa, utakuta mwana sio wako!! Ndicho kilichotokea kwa Juma Nature ambaye wazo lake la kuanzisha ndala liliendelea kuwa la mdomoni na ‘kutalk the talk’ ilhali Jokate Mwegelo akileta action kweli kwa ‘kuwalk the walk’. 


Baada ya mwanamitindo na mtangazaji Jokate Mwegelo kuanzisha ndala zake kupitia brand yake ya Kidoti, Juma Nature ambaye nae alikuwa na wazo hilo kwa muda mrefu, amefunguka na kusema Jokate amemgeza.

Akizungumza na 255 ya XXL, Clouds FM jana,Juma Nature amesema kuwa ingawa Jokate ametoa tayari ndala zake, naye pia ataingiza sokoni brand yake.

“Nani katoa we?”, alihoji Juma Nature aliyeonekana kutokuwa na habari hiyo. “Najua si msanii mwenzangu lakini inakuwaje! kama ametoa itakuwa ameiga nanihii yangu mimi fresh tu,mwache zimsaidie maisha, si idea yangu hiyo! Kutoa ni lazima nitoe kwasababu mimi naitwa Nature,Nature ni yule yule wa miaka na miaka,hatopotea hata kidogo. Mimi bado kidogo kwasababu na mambo mengi sasa hivi nafanya katikati hapa nadhani mashabiki wangu wakitaka kujua waangalie katika TV. Nadhani kila mtu anajua kwasababu gani? Hakuna msanii ambaye alishawahi kutangaza kwamba anategengeneza project ya ndala zaidi yangu.”

HALI INAZIDI KUWA MBAYA DARAJA LINALOTENGENISHA DAR NA BAGAMOYO LAVUNJIKA.

$
0
0


Daraja linalotengenisha Dar es salaam na Bagamoyo lililopo maeneo ya Bunju B limevunjika na kufanya kutokuwepo mawasiliano kati ya Dar na Bagamoyo....Nimepata habari kuwa mtu wa Bagamoyo akitaka kuja Dar lazima azungukie Kibaha.

MAFURIKO YAZIDI KUITESA JIJI LA DAR! ONA MAMBO YALIVYO KWA SASA.

$
0
0
Mburahati na Mayfair leo asubuhi.

Tokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo mbali mbali ya Dar esSalaam, zimepelekea uharibufu wa barabara na mazingira.

Haya ni maeneo ya jiji la Dar es Salaam yaliyoathirika na mvua inayoendelea kunyesha na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wakazi hasa wanaoishi bondeni au kwenye mkondo wa maji mfano mito.

VYAKULA VINAVYOONGOZA KUONGEZA AKILI KWENYE UBONGO.

$
0
0
BILA shaka ubongo ni miongoni mwa viungo muhimu vya binadamu lakini ni watu wachache sana wanaoutilia maanani. Ubongo ndiyo kiungo kinachohusika na utendaji kazi wote wa mwili na ndiyo unaowezesha mwili kuishi maisha ya furaha au karaha.
Hata hivyo, wakati mwingine utendaji kazi wa mwili unaweza kuwa siyo mzuri kutokana na sababu mbalimbali zinazoathiri ubongo, mojawapo ikiwa ni kukosekana kwa lishe bora na staili ya maisha inayotakiwa kuimarisha ufanisi wa ubongo.
Chakula ni moja ya sababu za msingi kabisa za kuimarisha ufanisi wa ubongo na kuzuia magonjwa mengine ya akili. Lakini kwa bahati mbaya watu wengi hawajui wale vyakula gani kwa lengo la kujenga akili na kuimarisha ubongo.
Ifuatayo ni orodha ya vyakula ambavyo vinaongoza kwa kuimarisha utendaji kazi mzuri wa ubongo:
MAFUTA YA SAMAKI
Mafuta ya samaki ni muhimu kwa ubongo na mfumo wa fahamu. Ulaji wa samaki wenye minofu kama samoni (salmon) na dagaa, utaweza kupata faida hizo kwa sababu aina hii ya samaki ina kiasi kingi cha mafuta ya Omega 3 ambayo huimarisha utendaji kazi na mawasiliano kati ya ubongo na seli za mwili moja kwa moja.
PILIPILI KALI
Pilipili kali nayo huwa ni chakula kikubwa cha ubongo kwa sababu ina kiwango kingi cha Vitamin C ambayo huhitajika zaidi kwenye ubongo, pilipili inaaminika kuwa na kiwango kingi cha vitamin hiyo kuliko hata machungwa.
MBEGU ZA MABOGA
Mbegu za maboga zina kiwango kingi cha madini ya ‘Zinc’ ambayo husadia kuongeza kumbukumbu (memory). Kuna njia nyingi za kula mbegu za maboga, moja wapo ni kuzikaanga na kula kama karanga, ukila kiasi cha kiganja kimoja kwa siku, inakuwa poa.
NYANYA
Nyanya ni muhimu sana kwa sababu huzuia magonjwa ya ubongo (brain disease) kutokana na kuwa na kirutubisho aina ya ‘Lycopene’ chenye uwezo wa kuzuia magonjwa nyemelezi yanayoweza kutokea. Hivyo ulaji wa nyanya utakusaidia kukupa kinga dhidi ya magonjwa mbalimbali, yakiwemo ya akili.
BROKOLI
Brokoli ni mboga ya majani aina fulani kama maua ya maboga, ambayo nayo inafaida sana kwenye ubongo, ina vitamin K, C na inatoa kinga ya mwili. Vitamin K inahusika moja kwa moja na utendaji kazi mzuri wa ubongo na husaidia kuzuia magonjwa yatokanayo na uzee.
KARANGA
Aina zote za karanga zina vitamin E, ambayo huzuia tatizo la upotevu wa kumbukumbu na pia zina mafuta yenye afya yanayohitajika mwilini.

MAYAI
Mwisho ni mayai ya kuku, ambayo yana kirutubisho aina ya Choline. Kirutubisho hiki huzalishwa mwilini kwa kiwango kidogo tu, hivyo kwa kula mayai (ya kienyeji) utaweza kuongeza kiwango cha kirutubisho hicho mwilini kwa kiwango kikubwa na hivyo kuimarisha afya ya ubongo.

WEMA NA DIAMOND SASA KWENDA MAREKANI.

$
0
0
Jamany wema sepetu atakufa kwa presha, baada ya msanii diamond the platnumz kupata show nchini marekani, wema sepetu aamua kumsindikiza mpenzi wake kwenye show.hiyo,
 
Gossip, yaani chini yacarpet inasemekana kuwa kuna warembo zaidi ya wa3 walishajiandaa na kuwekeana dau kuwa diamond the platnumz akitua tu marekani lazima watembee naye, But hapana chezea madame kasema safari hii wataula za chuya, kwa sababu tayari wema kashakata na kubuk mpaka na ticket, na kwaa taarifa yenu atapanda nae pipa kwenda kwenye show hiyo, so big up to wema sepetu hahah, haya madame abiria chunga mzigo wako.

Lady Jay Dee alazimika kuahirisha uzinduzi wa audio na video ya 'Nasimama'

$
0
0
Hali hiyo imemlazimisha Lady Jay Dee kuahirisha uzinduzi wa audio na video ya wimbo wake mpya alioupa jina la Nasimama.
Lady Jay Dee ametangaza kupitia ukurasa wake wa Facebook na kuambatanisha na picha ya jinsi eneo hilo lilivyoathiriwa na mvua.
Nasikitika kutangaza kuahirishwa kwa shughuli ya utambulisho wa wimbo na video mpya ya Jaydee 'NASIMAMA'. Kutokana na hali tete ya bojo iliojitokeza ambayo iko nje ya uwezo wa binadamu.. LAKINI Wimbo na Video vitarushwa LEO ktk mtandao. Çds na DVD vitasambazwa kwa walengwa((Media)) hapo kesho na Jumatatu.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote uliojitokeza....JayDee

The Game aamriwa kutomsogelea mama watoto wake baada ya kutuhumiwa kumpasua pua.

$
0
0
Kwa mujibu wa TMZ, April 2 rapper huyo aliamriwa kukaa umbali usiopungua takribani mita 100 kutoka kwa Tiffney lakini akapewa nafasi ya kuwatembelea watoto wake siku za wikendi pekee.
Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa tena mwezi huu.
Mwanzoni mwa mwezi huu, Tiffney Cambridge aliripoti polisi akimtuhumu The Game kumshambulia na kumpasua pua na kumsababishia majeraha mengine usoni.

Tazama Video Mpya ya Queen Darleen Feat. Shilole- Wanatetemeka.

$
0
0
Angalia video ya wimbo mpya wa Queen Darleen amemshirikisha Shilole, unaitwa Wanatetemeka.

Q Chilla aelezea ujio wake mpya na collabo za kimataifa alizofanya, anafanya kazi na producer mpya kutoka Lebanon.

$
0
0
Q Chilla ameiambia tovuti ya Times Fm kuwa amejipanga kurudi katika game kwa nguvu hivi karibuni na kwamba amemaliza hatua ya awali ya kuwaomba radhi wadau wa muziki ambao aliwakosea alipokuwa katika hali ya matumizi ya madawa ya kulevya.
“Mtu yeyote akiwa katika hali mbaya ya fikra potovu, kwenye madawa kwenye msongo wa mawazo anakuwa hayuko normal psychologically kwa hiyo vitu vingi vinaweza kutokea ukamuona ni mtu sio ambaye anafanana na wenzake. Kwa hiyo niliamia kwenye amani kuset mambo vizuri.” Amesema Q Chilla.
“Kwa hiyo nilikutana na wadau mbalimbali wa muziki kuzungumza. Jamani mimi ni ndugu yenu, naweza kuwa nimekosea hapa na pale lakini pia nahisi nina nafasi kubwa katika jamii na tasnia hii ya muziki. Na nina malengo na familia na watoto wananitazama.”
Ameeleza kuwa hata wale ambao hakuwafikia anaamini wamemsamehe pia na kwamba baada ya hapo alijisikia yuko huru na kuanza kuangalia project zake.
Mwimbaji huyo amesema ameshiriki katika kazi mbalimbali za kimataifa ikiwa ni pamoja na video aliyofanya na msanii mkubwa kutoka Ufaransa na amefanya production Ufaransa na kumalizia Zanzibar na kwamba iko katika hatua za mwisho.
“Halafu nikafanya video nyingine tena na msanii wa kimataifa toka Ethiopia Addis Ababa chini ya director mkubwa sana Afrika ambaye alinipa connection hii na akanishuti kwa gharama zake tukaenda Ethiopia lakini tunabidi tumalizie hapa shots za mwisho.” Ameeleza.
Hivi sasa mwimbaji huyo amepanga kutanguliza audio kati ya nyimbo mbili alizozitaja kuwa ni Red Carpet au Power of Love aliyofanya na producer mpya kwa Tanzania, mtanzania aliyekuwa akiishi Uingereza na Lebanon.
“Kuna producer mpya kutoka Lebanon amekuja hapa…amesoma Uingereza na Lebano lakini ni mtanzania ambaye anaishi Arusha, amekuja hapa amependa kazi zangu akasema ‘Q Chief naona unapenda sana kwenda International, naona una dream za kufika mbali. Nimekuwa nikifuatilia story ya maisha yako, ups zako and downs nahisi kwamba mzigo huu unaweza kukufikisha sehemu fulani. Kwa hiyo kuna mzigo unaitwa Power of Love unakuja.”

Kutana na Binti Wa Rais Kagame Ni Mmoja Ya Watoto Wazuri Wa Marais Africa.

$
0
0

Anaitwa Ange Kagame, ni mtoto wa pili na wakike pekee wa Rais wa 6 wa Rwanda Paul Kagame, mama yake anaitwa Jeannette Nyiramongi na ndiye first lady wa Rwanda.

Ange hajalelewa nchini Rwanda, ameishi maisha yake yote nje ya nchi. Wanafunzi waliosoma naye wanasema binti huyu anajituma sana kwenye masomo na kusaidia watu na muda mwingi hutumia kufuatilia mambo yanayoendelea nyumbani kwao Rwanda.
Kwa sasa Ange amerudi Rwanda na anafanya kazi nyingi za kujitolea kwa jamii kama kuoanda miti, kampeni za kupiga vita magonjwa nguli Rwanda na kuendesha makundi ya kukomboa wanawake kutoka kwenye umasikini.
k 1 k 4 k 5


Viewing all 2632 articles
Browse latest View live