Quantcast
Channel: D'JARO ARUNGU
Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Msomalia aliyeigiza kwenye filamu ya 'Captain Philips' amefilisika kabisa.

$
0
0

Raia wa Somalia ambaye aliingia Marekani akitokea Somalia alikokimbia vita, Barkhad Abdi na mwisho kujikuta amegeuka kuwa miongoni mwa mastaa wa Hollywood baada ya kufanya vizuri katika filamu ya Captain Phillips amefilisika kabisa.

Barkhad Abdi ambaye mbali na mkwanja mrefu alioingiza kupitia filamu ya Captain Phillips aliyoigiza kama mkuu wa haramia, aliwahi kulipwa kiasi cha dola 65,000 baada ya kuwekwa kwenye orodha ya waigizaji wanaowania tuzo za Oscar, bado ameonekana akiweweseka kiuchumi japo hajafikia hali ile aliyotoka nayo Somalia.
Inasemekana kuwa kwa hivi sasa ana wakati mgumu katika kuhakikisha anaweza kumudu maisha ya level za Hollywood ambayo alianza kuyaishi baada ya kukabithiwa uhusika wa filamu hiyo iliyowahusisha mastaa wa Hollywood.
Abdi ameweza kupata nafasi nyingine ya kuigiza katika filamu kubwa kama mwanariadha mkongwe wa Afrika Kusini, Willie Mtolo  ambayo inaitwa ‘The Place That Hits The Sun, na huenda hiyo ikamuokoa kutoka kwenye msoto.
Muigizaji huyo alihudhuria pia katika tuzo za Oscar za mwaka huu na kuwa na muonekano sawa na wale wa Hollywood japo mfuko wake hauko sawa.
Mbali na tuzo za Oscar, aliwahi pia kutajwa kuwania tuzo za Golden Globes kama ‘Muigizaji bora msaidizi’.

Viewing all articles
Browse latest Browse all 2632

Trending Articles