
Ligi kuu nchini England imeendelea hii Jana kwa michezo iliyopigwa kwenye viwanja kadhaa ambapo mchezo uliochezwa uwanja wa St. James Park, Newcastle United walishinda mchezo wao wa tatu mfululizo wakiwafunga Liverpool kwa bao moja kwa sifuri mfungaji akiwa Ayoz Perez dakika ya 73.

Arsenal imewafunga Burnley mabao 3- 0 kwenye uwanja wa Emirates, huku Chelsea wakishinda mchezo wao dhidi ya wapinzani wao Queens Park Rangers kwa matokeo ya mabao 2 – 1.

Southampton waliwafunga Hull City 0-1 , West Brom nao wakawafunga Leicester City 0-1 , Everton na Swansea wakatoka sare ya bila kufungana huku West Ham United na Stoke City wakitoka sare ya 2-2.
Haya ndiyo matokeo ya ligi hiyo kwa kWA jana.
Newcastle1 – 0 Liverpool FT
Arsenal 3 – 0 Burnley FT
Chelsea 2 – 1 QPR FT
Everton 0 – 0 SwanseaFT
Hull 0 – 1 Southampton FT
Leicester 0 – 1 West Brom FT
Stoke 2 – 2 West Ham FT