
Alilazimika kutazama TV hizo kwa umakini baada ya kuona shangwe walilopata WEUSI ambapo mashabiki walikua wanaimba nyimbo zao kwa muda mrefu ambapo Davido kabla ya kuuliza alitumia muda mrefu kuwatazama kwa makini baada ya kushangazwa na shangwe walilokua wanapata WEUSI hawa.

Hii itafanya idadi ya Wasanii wa bongo wanaofahamika na Davido iongezeke manake alipokuja juzi Tanzania alihojiwa muda mfupi tu baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege na kusema msanii pekee wa Tanzania anaemfahamu ni Diamond Platnumz.
Mengine aliyoyasema ni kwamba kwenye album yake mpya inayotoka mwanzoni mwa 2015 wameshirikishwa wasanii wachache kutoka Afrika ambao ni pamoja na Diamond na Mafikizolo na kwamba kuna wasanii wawili wakubwa wa kimataifa aliowashirikisha ambao hatowataja kwa sasa.